What Dunia wants to say/Swahili text

Kwanza – natowa shukrani kwa mwaliko wenu

Pili – tunashukuru kwa mapokezi mazuri  (kuanzia mwanzo hadi mwisho)

Tatu – Tumeanza ziara yetu kutembelea umoja wa manispaliti na kupata maelezo ambayo tumeyapenda sana.

Nne – Tumetembelea kiwanda cha mikate na kiwanda cha mbao. Tumependa sana

Tano – Nimevutiwa na kazi za wajasiriamali jinsi wanavyoshirikiana katika kutafuta maisha. Wajasiriamali hawa ni watu wazima lakini bado wanajishughulisha na kazi za kuzalisha mali badala ya kukaa nyumbani

Tulitembelea Makumbusho ambako tulifahamishwa shughuli za vijana hasa baraza la vijana linavyoendeshwa. Pia tulikutana na rafiki wa Makunduchi na kuwaelezea Makunduchi tunayotaka iwe.

Tulitembea skuli na kuona ufundishwaji na mashirikiano baina ya wazee na skuli ambayo ni mazuri na hivyo kusaidia ufaulu wa wanafunzi.

Vile vile tulienda kwenye mchezo wa kuangusha chumba kwa kutumia mpira mzito “bowling” Mchezo huu tumeupenda sana na kuufurahia na natamani na sisi tufanye ili kiwe kivutio cha watu wazima.

Pia tunawashukuru wote waliotuandalia vyakula vya aina mbali mbali na kututembeza maeneo tofauti. Ahsanteni sana.

Mwisho tunatoa pongezi kwa uongozi wote wa Sundsvall . Tunaomba tuzidi kuwa na mashirikiano mema. Udumu umoja wetu. Tupendane, tushirikiane, tusaidiane. Ahsanteni. 

1 thought on “What Dunia wants to say/Swahili text

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.